Kiswahili Quick guide to Talk to Loop

Talk to Loop ni chombo cha maoni kilicho salama, rahisi kufikia, cha kidijitali na huru kwa jamii zilizoathirika na majanga. Kinawawezesha watu kutoa maoni kwa lugha yao, kwa wakati wanaopendelea, na kupitia kifaa walichozoea.

Kinawawezesha pia mashirika, katika sekta zote, kujibu na kuchukua hatua kulingana na maoni ya jamii kwa wakati halisi. Kina sifa za kipekee zinazokifanya kitofautiane na mifumo mingine ya kupokea maoni, ikiwemo:

Jinsi Talk to Loop inavyofanya kazi

Watu husikia kuhusu Talk to Loop kupitia vyanzo vya karibu kama wafanyakazi, redio, vipeperushi vinavyosambazwa na mashirika mbalimbali, na pia kwa njia ya mdomo. Wanaweza kutoa maoni kwa sauti, SMS, WhatsApp, Facebook Messenger, Telegram, au kupitia tovuti kwa lugha wanayoipendelea. Kwa sasa, Loop inasaidia lugha sita na inaweza kuongezwa hadi zaidi ya lugha mia moja.

Maoni hushughulikiwa ndani ya saa ishirini na nne: huandikwa, tafsiriwa, hutajwa na kupelekwa, ili mashirika yapokee taarifa kwa wakati halisi na kujibu haraka. Wakaguzi pia hutafsiri na kufikisha majibu kupitia njia na lugha ambazo watumiaji wamechagua.

Taarifa nyeti, kama unyanyasaji au ufisadi, hazichapishwi kwenye jukwaa la wazi. Zinashughulikiwa kando na kwa usiri na wataalamu wa ulinzi, kwa kufuata njia salama na zinazolenga waathirika, na hatua maalum za ziada hufuata ili kuhakikisha usalama na heshima kwao.

Mara tu kesi inapowasilishwa na kurejelewa, Wahariri Wataalamu wa Maoni Nyeti hufuatilia na wanajamii. Kwa maelezo zaidi, angalia Mfumo wetu wa Kushughulikia Maoni Nyeti.

Kwa kufanya maoni yawe salama, kupatikana kwa urahisi, na yenye kuleta hatua, Talk to Loop inachangia ujumuishaji wa sauti za jamii katika kufanya maamuzi, kwa lengo la kuleta mabadiliko ya maana na ya kudumu.

Takwimu zilizokusanywa kwenye jukwaa la wazi zinatoa nafasi ya kuchambua taarifa kulingana na makundi ya watu, maeneo na mada. Data ya wazi na isiyo na majina inaweza pia kuunganishwa na seti nyingine za data, na hivyo kuimarisha maamuzi yanayotegemea takwimu duniani kote.

Taarifa zote za wazi hushughulikiwa kwa makini ili kupunguza upotoshaji au maudhui yasiyofaa. Ingawa hatuchunguzi au kuthibitisha madai, malalamiko makubwa hayatawekwa hadharani na hutumwa kwa siri kwa watu maalum walioteuliwa, kwa kufuata taratibu kali za uwasilishaji na kwa msingi wa ruhusa ya mwandishi.

Kipaumbele chetu ni usalama na ulinzi wa watumiaji. Tunakusudia kupata imani ya sekta na jamii kwa kutenda kazi kwa njia huru. Jukumu letu ni kufikisha maoni ya jamii kwa usalama kwa watu sahihi na kisha kujiondoa, ili uwajibikaji na hatua vitokee.

Tunatumia Sera madhubuti ya Faragha inayohakikisha ruhusa ya watumiaji na usimamizi salama wa data. Tunakusanya data ya hiari pekee, kulinda taarifa za mawasiliano, na kuzuia kuchapishwa kwa maelezo yanayotambulika kwa mfanya jina an nambari ya simu. Hatuzui data, na watumiaji wanaweza kuomba data yao kufutwa wakati wowote. Data huhifadhiwa kwenye seva za AWS zinazokubaliana na GDPR na zenye viwango vya juu vya usalama; na tunashirikiana na mitandao ya simu ya ndani chini ya makubaliano madhubuti ya Ulinzi wa Data. Kwa maelezo zaidi, angalia DPIA.

Kwa Nini Talk to Loop Ni Muhimu?

Hatua za sasa za uwajibikaji na ulinzi hazisaidii jamii ipasavyo. Ushahidi unaonyesha kuwa mbinu bunifu zinahitajika ili kushinda changamoto za mfumo na kutoa zana zinazoweza kufikiwa kwa urahisi, zinazojibu kwa haraka, zinazoendelea kwa muda mrefu na zinazoweka sauti za jamii katikati.

Mabadiliko ya mfumo yanahitaji maamuzi ya pamoja yanayotegemea takwimu, huku sauti za jamii zikipewa kipaumbele. Kwa kukusanya data kutoka kwa washirika, sekta, maeneo, hatua na makundi ya watu yaliyoathirika, Talk to Loop inaweza kutoa ufahamu kuhusu mwenendo wa jumla badala ya matukio au miradi ya pekee. Mashirika ya kitaifa, mashirika ya kimataifa na INGOs, miongoni mwa wengine, wanaweza kutumia Loop na data inayotokana nayo.

Ahadi za kimataifa kuhusu hatua za haraka, zenye uwajibikaji na zinazojikita kwa jamii zinahitaji zana zilizo wazi, zinazoshirikisha wadau na zinazohakikisha uwajibikaji. Talk to Loop inalingana na mipango mikuu ya misaada ya kibinadamu duniani, kama makubaliano ya Grand Bargain yanayosisitiza ushiriki na kuweka jamii katikati, pamoja na mpango wa Emergency Relief Coordinator’s Flagship Initiative unaolenga uwajibikaji kwa jamii zilizoathirika. Talk to Loop ni chombo cha vitendo kinachoweza kutumiwa na wadau wote kupata ufahamu wa maana na kufuatilia uwajibikaji kwa wakati halisi.

Hadi sasa, Talk to Loop imepata mafanikio gani?

Kuanzia mwaka 2021 hadi 2024, Talk to Loop imesimamia vipande 4,000 vya maoni na kushughulikia taarifa nyeti 144 kutoka Ukraine, Poland, Ufilipino, Indonesia, Zambia na nchi nyingine. Kati ya hizi, asilimia 100 zimefungwa rasmi. Pia tulipeleka kesi 40 kwa msaada zaidi na madai 38 (udanganyifu, ufisadi, ukiukaji wa maadili, unyanyasaji wa kingono (SEA) na malalamiko mengine ya huduma). Katika kipindi hiki, mashirika 838 kutoka nchi 25 yalisajiliwa na Talk to Loop.

Kwa sasa jukwaa linafanya kazi ndani ya Somalia na Somaliland (kwa kutumia nambari fupi (shortcode)) na linazinduliwa Ethiopia na Kenya, huku majadiliano yakiendelea kuhusu uwezekano wa kupanuka hadi DRC. Pia linafanya kazi kimataifa kupitia Tovuti na WhatsApp kwa Kiingereza, Kiarabu, Kihispania na Kifaransa.

Tangu mwaka 2022, Talk to Loop imekuwa inapatikana Somalia na Somaliland na hadi sasa imepokea zaidi ya vipande 22,000 vya maoni, karibu simu 333,000, na kusimamia takribani taarifa nyeti 3,700, huku mashirika zaidi ya 129 yakiwa yamesajiliwa.

Una nia ya kutumia au kusaidia Talk to Loop?